Maofisa Habari kutoka Wizara mbalimbali, waliohudhuria kikao kazi cha maofisa habari mjini Dodoma, wakiwa katika majadiliano ya vikundi kuhusu mafanikio na changamoto zinazoyakabili maeneo yao, ya kazi, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Luteni Kanali Juma Sipe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Serikalini, Wizara ya Ulinzi.
Na Aron Msigwa, Dodoma
5/2/2013,
Kikao kazi cha Maofisa Habari wa Serikali kutoka Wizara, taasisi,
Wakala wa Serikali, Mashirika ya umma, Mikoa na Wilaya
mbalimbali nchini leo, kimeingia siku ya pili mjini Dodoma kwa
maofisa hao kupata fursa ya kujadili changamoto zinazokabili
vitengo vya habari na mawasiliano serikalini na namna ya
kuzitatua.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo ile
ya Mwongozo wa Ofisi za Mawasiliano serikalini iliyowasilishwa
na Mkurugenzi wa Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO)
anayeshughulikia uratibu wa vitengo vya mawasiliano serikalini
akitoa msisitizo mkubwa kwa maafisa habari kuyafahamu vizuri
majukumu yao ya kazi kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa
umma ili kuboresha utendaji wa kazi.
Pia maafisa hao wamepata fursa ya kujifunza namna ya kuboresha
mawasiliano serikalini kupitia mada ya mkakati wa mawasiliano
(Communication Strategy) wa kuiwezesha jamii kupata taarifa
sahihi kwa muda muafaka ,mada iliyowasilishwa na Meneja
mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Bw. Innocent Mungy.
Katika mada hiyo Bw. Mungy ametoa wito kwa maafisa hao
kuzitumia nafasi zao kutoa taarifa kwa umma mara kwa mara ili
kuwapa fursa wananchi kufahamu yale yanayofanywa na
serikalini.
Ametoa wito maafisa hao kushirikiana na vyombo mbalimbali vya
habari katika kutekeleza mkakati huo kwa kuhakikisha kuwa
wanatoa habari kwa umma kupitia radio, magazeti, televisheni na
mitandao ya kijamii ili kuepusha madhara yanayoweza
kusababishwa na jamii kukosa taarifa sahihi za serikali za
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.
|
Tuesday, February 5, 2013
Kikao kazi cha Maofisa Habari wa Serikali, Mjini Dodoma, chaingia siku ya pili, Changamoto mbalimbali zaibuliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment