Mwenyekiti wa Kamati ya Uwasilishaji wa mapendekezo ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu, David Nyendo (kushoto), akiwasilisha maoni ya kamati hiyo, kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao, uliofanyika leo, Jumatano Feb. 13, 2013, Ofisi za Makao Makuu ya tume, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Dk. Salim Ahmed Salim.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia), akizungumza na wawakilishi wa makundi ya jamii ya watu wenye ulemavu, ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Nyendo (kushoto), mara baada ya kufika Makao Makuu ya Tume leo, Jumatano, Feb. 13, 2013, kuwasilisha mapendekezo yao, juu ya  muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dk. Salim Ahmed Salim.

Mkalimani wa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania (UMVITA), Ruth Hope akisaidia uelewa wa lugha ya mawasiliano kwa watu wa jamii ya watu wenye ulemavu wa kusikia katika mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo jijini Dar es Salam. Walemavu hao waliunda Kamati iliyokutana na Tume ili kuwasilisha mapendekezo yao, juu ya  muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii yao. (Picha zote na Tume ya Katiba)