TANGAZO


Wednesday, February 13, 2013

Katibu wa Bunge atoa ufafanuzi wa Mkutano wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, akira baadhi ya Wabunge kukiuka Kanuni



Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashilila, akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya Wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa Bunge, uliomalizika mjini Dodoma hivi karibuni na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya Kamati kuondolewa  pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3, zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (Picha zote na Aron Msigwa)
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashilila, akitoa somo kwa waandishi wa habari, kuhusu umuhimu wa Wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo, kanuni za Bunge ili kuondoa manug'uniko yanayojitokeza pindi wanapozuiliwa na Spika kuchangia mijadala au kutoa hoja bungeni kwa sababu ya kukiuka kanuni na umuhimu wa waandishi wa habari  kuzitumia taarifa rasmi za Bunge katika utoaji wa taarifa zao.

Waandishi wa habari, wakiendelea kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za Bunge kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, Dar es Salaam leo. Pamoja na mambo mengine, amesema Ofisi yake, itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za Bunge pamoja na uandaaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge. 

No comments:

Post a Comment