Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi (aliyeiyanyua juu), tuzo ya Mbuga ya Wanyama ya Serengeti, mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo, kuwa ni moja ya Maajabu Saba ya Asili katika Bara la Afrika, Hoteli ya Mount Meru. Kushoto ni Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders, Philip Imler. Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya Utalii, ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crater na Mbuga ya wanyama ya Serengeti. Hafla hiyo, imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanyabiashara, Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau mbalimbali wa Utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crater, muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders, Phillip Imler, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza Maajabu Saba ya Asili ya Afrika, iliyofanyika jana jioni, Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.
Vikundi vya ngoma kutoka makabila ya Mkoa wa Arusha vikiwa tayari kuburudisha katika hafla hiyo, kama vinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB, ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Dk. Aloyce Nzuki, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa. Kushoto ni Mbunge Shah wa Mafia, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya hiyo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini, wakiwa katika hafla hiyo.
Mbunge James Lembeli, akisalimiana na Mike Teyrol, walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki marufu, Mrisho Mpoto 'Mjomba' na kundi lake, wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devitha Mdachi, akiwa pamoja na Maofisa wengine wa bodi hiyo, wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi Maimuna Tarishi. Katikati ni msaidizi wake, Miskanji.
Kikundi cha ngoma za asili, kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwa Meza Kuu pamoja na viongozi wengine, wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders, jijini Arusha jana jioni. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Waziri wa Utalii wa Uganda, Agness Agunyu na kushoto ni mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders, Philip Imler na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akiwasikiliza Wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo, Deo Filikunjombe (kulia) na kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini, Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili Hoteli ya Mount Meru kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kushoto), akiwa katika hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dk. Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi wa nchi mbalimbali, waliohudhuria katika hafla hiyo, wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo. Wa kwanza kulia ni Balozi Mutinda Mutiso wa Kenya, nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dk. Aloyce Nzuki, akiongea katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi (kushoto), akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crater, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA, Allan Kijazi katika hafla hiyo. Kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA, Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
Mwanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders, Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, ikapokelewa na Mhifadhi wa mlima huo. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kushoto ni Philip Imler.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania (kulia), akizungumza na Balozi Charles Sanga, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) na Mkurugenzi wa bodi hiyo, Dk. Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment