TANGAZO


Wednesday, February 13, 2013

Rais wa Zanzibar, Dk. akabidhi Vitambulisho vya Taifa,awamu ya Kwanza visiwani Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Vitambulisho vya Taifa, Dicson Maimu, alipowasili Viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Chukwani, nje ya mji wa Zanzibar leo, katika hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea Kitambulisho cha Taifa kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima, wakati wa hafla ya Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Chukwani, nje ya mji wa Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji, akiweka kidole Gumba kwa ajili ya kufanya uhakiki katika mashine maalum, wakati wa hafla ya Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, akiweka kidole Gumba kwa ajili ya kufanya uhakiki katika mashine maalum, wakati wa hafla ya Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya viongozi na wananchi na wafanyakazi wa Mamlaka ya vitambulisho, wakiwa katika hafla ya utoaji wa vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, hafla iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi, Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania (JWTZ), Jenerali Devis Mwamunyange, akiweka kidole Gumba kwa ajili ya kufanya uhakiki katika mashine maalum, wakati wa hafla ya Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka kidole Gumba kwa ajili ya kufanya uhakiki katika mashine maalum, wakati wa hafla ya Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na kushoto ni Afisa Vitambulisho, Abdalla Mmanga Omar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akimkabidhi kitambulisho Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akimkabidhi kitambulisho, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, wakati wa hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akimkabidhi kitambulisho, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, wakati wa hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akimkabidhi kitambulisho, mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, wakati wa hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akimkabidhi kitambulisho, mke wa Makamo wa Pili wa Rais, Mama Asha Balozi Seif, wakati wa hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa, awamu ya kwanza kwa upande wa Zanzibar, iliyofanyika leo, Viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje ya Mji wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment