TANGAZO


Wednesday, February 13, 2013

Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga yaikung'uta African Lyon mabao 4-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam


Mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga, akiudhibiti mpira huku akibanwa na Mohamed Samatta wa African Lyon, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 4-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Sunday Bakari wa African Lyon, akijaribu kumzuiya David Luhende (nyuma) wa Yanga, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 

 Mashabiki wa Yanga, wakifurahia timu yao wakati ilipokuwa ikimenyana na African Lyon leo jioni.

Ilikuwa ni furaha na nderemo kwa mashabiki wa timu ya Yanga kutokana na timu yao kuzidi kujikita katika kilele cha Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuiadhibu African Lyon mabao 4-0 kwenye mchezo huo.
Kocha wa Yanga, Ernst Brandts (kulia), akiwa na wachezaji wake wakati wakijipoza kwa maji, uwanjani hapo, wakati wa mchezo huo na African Lyon.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro 'Majeshi', akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo, wakati walipokuwa wakijipatia maji ya kunywa, wakati wa mchezo huo leo jioni Uwanja wa Taifa.

Kocha wa Yanga, Ernst Brandts (kulia), akitoa maelekezo kwa mchezaji wake, Frank Domayo, wakati alipokuwa akijipoza kwa maji, uwanjani hapo, katika mchezo huo na African Lyon.
Wachezaji Haruna Niyonzima na Simon Msuva (katikati), wote wa Yanga, wakimpongeza Jeryson Tegete baada ya kuifungia timu hiyo, bao la kwanza dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 

No comments:

Post a Comment