Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini, Dar es Salaam. (Picha zote na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, Jaji January Msofe, Spika Anne Makinda, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadik leo, Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, leo Februari 6, 2013 baada ya Rais, kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Kushoto ni Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.
Viongozi wa dini ya Kihindu wakielekea kwenye kipaza sauti ili kuomba dua leo Februari 6, 2013, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo pia walishiriki kwenye maadhimisho hayo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufaa, leo Februari 6, 2013, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wakuu wastaafu, viongozi wa Wizara ya Sheria na Katibana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiq (wa tatu kulia, nyuma), leo Februari 6, 2013, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu, Rais wa Mawakili, leo Februari 6, 2013, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.
No comments:
Post a Comment