TANGAZO


Wednesday, February 6, 2013

Taifa Stars yapiga Cameroon bao 1-0, mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam

Mchezaji Assou Ekotto wa timu ya Taifa ya Cameroon, akimtoka Mrisho Ngassa wa Taifa Stars, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni. Stars imeshinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Erasto Nyoni (4) wa Taifa Stars na Bedimo Henri wa Cameroon wakiwania kuudhibiti mpira katika mchezo huo.
Erasto Nyoni wa Taifa Stars na Bedimo Henri wa Cameroon wakiwania kuudhibiti mpira katika mchezo huo.
Erasto Nyoni wa Taifa Stars na Bedimo Henri wa Cameroon wakiwania kuudhibiti mpira katika mchezo huo, huku Salum Abubakar wa Stars, akikimbilia kwa ajili ya kutoa msaada.
Erasto Nyoni wa Taifa Stars na Bedimo Henri wa Cameroon wakiwania mpira huo.

Nyoni wa Taifa Stars, akionekana kumzidi Henri wa Cameroon katika vita hiyo ya kuwania mpira huo.

Tchami Herve (20) wa Cameroon, akiudhibiti mpira huku akiwekwa chini ya ulinzi mkali na Erasto Nyoni wa Taifa Stars.
Erasto Nyoni wa Taifa Stars, akiendelea kumdhibiti Tchami Herve wa Cameroon.
Erasto Nyoni (kulia) wa Taifa Stars na Eloundu wa Cameroon, wakikimbilia mpira kuelekea lango la Stars.
Salum Abubakar wa Taifa Stars, akimtoka Makoun Thierry (13) wa Cameroon, katika mchezo huo.
Eloundo wa Cameroon, akiudhibiti mpira huku akitafuta mbinu ya kumtoka Salum Abubakar wa Taifa Stars, nyuma yake.
Wachezaji wa Taifa Stars wakihimizwa kurejea uwanjani na refarii wa mchezo huo (kulia), wakati walipokuwa wakishangilia goli pekee katika mchezo huo, lililofungwa na Mbwana Samatta (10), wanayempongeza.
Ubao wa matangazo hadi dakika ya 91, ulikuwa ukisomeka Tanzania 1, Cameroon 0 baada ya mchezaji Mbwana Samatta kuifungia timu hiyo bao katika dakika ya 88 ya mchezo huo.
Wachezaji wa Stars wakimshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kufaniki kuilaza Cameroon bao 1- 0.
Wachezaji wa Stars, wakiwa wamemaliza kumshukuru Mungu, baada ya kumalizika kwa mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufaniki kuilaza Cameroon bao 1- 0.
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, akimpongeza Amri Kiemba wa Stars baada ya kumalizika mchezo huo jioni hii, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Watanzania waliokuwepo Uwanja wa Taifa, wakifurahia ushindi huo, huku wengine wakinyanyua mabango waliyoandika ujumbe mbalimbali wa kusifu timu yao hiyo.

No comments:

Post a Comment