Timu ya Nigeria, Super Eagles, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuilaza Ivory Coast 2-1.
Katika mpambano huo, Ivory Coast ndiyo iliyokuwa ikipewa nafasi zaidi kufuatia kikosi chake kusheheni majina makubwa kama vile Didier Drogba, Yaya Toure, Emmanuel Eboue, Gervihno, Kolo Toure, Cheick Tiote, Salomon Kalou na wengine wengi ndiyo yaliyowapa mashabiki wa timu ya Ivory Coast matumaini ya kusonga mbele.
Ivory Coast ilisawazisha bao hilo baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Drogba na kumfikia mfungaji Cheick Tiote katika dakika ya 51 na kuunganisjha kwa kichwa mpira huo.
Hata hivyo Nigeria ilipata bao lingine la pili katika dakika ya 78 likifungwa na Sunday Mba. Kosa la safu ya ulinzi ya Ivory Coast kumwaachia mfungaji kukokota mpira kwa muda mrefu ndiko kulikopeleka kilio kwa vijana wa Ivory Coast.
Kikosi cha Ivory Coast ambacho kilionekana kuwa ni bora zaidi katika michuano hii, kimeonekana kuendelea na mkosi wake kama ilivyokuwa mwaka jana wakitolewa katika fainali na Zambia, timu ambayo haikupewa nafasi.
Wachezaji wengi wa Ivory Coast kama vile Didier Drogba, Kolo Toure, Zokora na wengine wenye majina makubwa , huenda mashindano haya yalikuwa ya mwisho katika kuchezea timu yao ya taifa, kwani watakuwa na umri mkubwa na hivyo kutoshiriki michezo kama hii mwaka 2015.
Mchezo unaofuata ni kati ya Burkina Faso na Togo kukamilisha michezo ya robo fainali. Timu zilizosonga mbele ni pamoja na Ghana, Mali na Nigeria, huku timu ya nne ikitoka katika mpambano kati ya Burkina Faso na Togo.
No comments:
Post a Comment