TANGAZO


Thursday, February 21, 2013

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid afungua Kongamano la NHIF na wanahabari, mjini Mtwara

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti, alipowasili katika Chuo cha Ualimu Mtwara, kufungua Kongamano la Nane la huo wa NHIF na Wanahabari mjini Mtwara leo. 

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la NHIF na Wanahabari, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, wakati alipokuwa akilifungua kongamano hilo, mjini Mtwara leo.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akizungumza wakati alipokuwa akilifungua  Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya (NHIF) na Wanahabari, mjini Mtwara leo. 

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akitoa shukrani zake kwa niaba ya wanahabari baada ya Naibu Waziri  wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kulifungua kongamano hilo, mjini Mtwara leo.

Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, mkoani Mara, Geaorge Marato, akielezea jinsi walivyofanya utafiti kuhusu matumizi ya fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya NHIF na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), katika Wilaya za Rorya na Serengeti, mkoani Mara. Utafiti huo, ulifanywa na mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, Saidi Mwishehe.

No comments:

Post a Comment