TANGAZO


Sunday, February 3, 2013

Mwaka Mpya wa Kichina kukaribishwa usiku wa leo jijini Dar es Salaam


Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin nchini China, Zhang  Junfang (kushoto), akikabidhi picha ya kiutamaduni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, wakati alipomtembelea leo, ofisini kwake, jijini Dares Salaam, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania. Meya huyo, yupo nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina, zitakazo adhimishwa leo jioni, katika Viwanja vya Mnazi  Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin kutoka China, Zhang  Junfang (watatu kushoto), akifurahi baada ya kumvalisha Waziri Mukangara, kitambaa (skafu), chenye michoro ya utamaduni wa China leo, jijini Dar es Salaam. Meya huyo yupo nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zitakayofanyika leo jioni, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin nchini China, Zhang  Junfang (katikati), akimvisha kitambaa chenye michoro ya  kiutamaduni, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, wakati apomtembelea leo, ofisini kwake, jijini Dares Salaam, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania. Meya huyo yupo nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina, zitakazoadhimishwa leo jioni, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Meya huyo, akizungumza na Waziri wa habari, alipomtembelea leo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.  (Picha zote na Magreth Kinabo - Maelezo)

No comments:

Post a Comment