TANGAZO


Saturday, February 2, 2013

Matukio ya Bunge, mjini Dodoma


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akijibu hoja ya Wizara, ya Mbunge Yussuf Haji Kahamis  (Nugwi ), hayupo pichani, kuhusu Serikali ina mikakati gani kwa wanamichezo wetu juu ya ugonjwa wa moyo, ambao ni tishio kubwa kwa maisha yao jana, Bungeni- Dodoma.
Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akichangia na kuunga mkono hoja  ya Mbunge wa  Nzega,  Dk. Hamis Kigwangala ya kuitaka Serikali ianzishe mpango maalumu wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha Mfuko wa Mikopo ya Vijana wanaowekeza kwenye Kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo, Feb. 1, 2013, mjini Dodoma jana.
  Wabunge Mussa Azzan 'Zungu' (Ilala) na wa Mafia, Abdulkarim Shah (kulia), wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
Makatibu wa Bunge wakifuatilia hoja mbalimbali  katika  mkutano wa Kumi Bungeni – Dodoma.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akichangia hoja katika Bunge- Dodoma.
Wabunge Mwingulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Ismail Rage (kulia), wakizungungumza hoja mbalimbali katika  viwanja vya Bunge- Dodoma jana.
Wabunge, kutoka kulia, Hezekiah Chibulunje (Chilonwa), Said Arfi (Mpanda Mjini) na Mohamed Missanga ( Singida Magharibi), wakisikiliza maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na benki ya NMB nchini kutoka kwa  Meneja mikopo wa NMB, Susan Shuma (kushoto), katika maonesho kwenye viwanja vya Bunge – Dodoma.

Wabunge Vicky Kamata, Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene (MP), wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge.

No comments:

Post a Comment