TANGAZO


Monday, February 4, 2013

Dk. Mukangara afungua kikao kazi cha Maofisa Mawasiliano

Picha-no-11.jpg
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akizungumza katika moja ya mikutano yake.

Na mwandishi wetu, Dodoma
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ameagiza Wizara, Taasisi za Serikali, Wilaya na Mikoa kwamba  lazima Maofisa Habari  na Mawasiliano wawe sehemu ya Menejimenti katika maeneo yao, ili waweze kuisemea Serikali kwa ufasaha.

Akifungua Kikao Kazi  cha Maofisa Habari na Mawasiliano, Mjini Dodoma leo, Dk. Finella Mukangara, alisema kuwa, ili Maofisa Habari waweze kuisemea Serikali lazima waweze kushiriki katika maamuzi ya msingi ya taasisi husika na kutoa ushauri ipasavyo.

"Ninyi kama Wasemaji wa Taasisi zenu, lazima muwe sehemu ya Menejimenti katika maeneo yenu ili muweze kutoa ushauri unaotakiwa katika.... ", alisema.

Aidha, amewataka Maofisa Habari na Mawasiliano kutoka vyombo vya Umma kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuelezea jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kueleza kwamba Serikali inafanya masuaka ya maendeleo lakini uwezo wa kuyasemea umekuwa ni mdogo.

Sambamba na hilo, Waziri alisema ni vema vitengo vya Habari katika ngazi zote kuhakikisha kwamba vinaimarishwa kwa maana ya kuwajengea uwezo maofisa wao pamoja na kuwa na nyenzo za kufanyia kazi.

Aliwataka Maofisa Habari kutaka kujiendeleza kielimu ili waweze kufanya kazi zao ni kwa weledi na umahiri mkubwa katika maeneo yao ya kazi. Alisisitiza kwamba angalau Ofisa Habari awe na kiwango cha elimu cha ngazi ya Digrii.

No comments:

Post a Comment