TANGAZO


Monday, February 4, 2013

Rais Kikwete akagua ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi, lililopewa jina lake, mkoani Kigoma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Mama Salma Kikwete, wakikagua ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi lililopewa jina la Daraja la Kikwete, mkoani Kigoma leo, Februari 4, 2013. Asilimia zaidi ya 90 ya ujenzi wa daraja hilo, umekamilika na linatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka huu. (Picha zote na Ikulu)
Wataamu wa ujenzi wa Daraja hilo, wakimpatia maelezo kuhusu ujenzi huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati alipokwenda kukagua ujenzi wake, daraja lililopewa jina lake. Kushoto kwa  Rais ni mkewe, Mama Salma. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Mama Salma Kikwete na Maofisa mbalimbali, wakikagua ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi, lililopewa jina la Daraja la Kikwete, mkoani Kigoma leo, Februari 4, 2013. Asilimia zaidi ya 90 ya ujenzi wa daraja hilo, umekamilika na linatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, John Ndunguru, akimuonesha jambo Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina lake. Nyuma ya Rais ni mkewe, Mama Salma. 

No comments:

Post a Comment