TANGAZO


Monday, February 4, 2013

Mkurugenzi wa UNESCO atembelea Mji Mkongwe, Zanzibar

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova (wanne kutoka kushoto), akitembelea sehemu za Mji Mkongwe wa Zanzibar  leo, ikiwa ni miangoni mwa ziara yake ya siku mbili Kisiwani Zanzibar. (Picha zote na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar)
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova (kushoto), akiangalia utamaduni wa ususi wa kindu, ambazo hutengenezewa vitu mbalimbali, ikiwemo makawa, mikeka na hata mikoba katika moja ya maduka, alioingia katika sehemu za Mji Mkongwe, ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya siku mbili kisiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova (kushoto), akipata maelezo ya vitu vinavyotengenezwa kwa kutumia kombe za Pwani kutoka kwa Meneja wa duka la Fahari Zanzibar, Azza Salum katika moja ya maduka aliyoingia katika sehemu za Mji Mkongwe, ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya Siku mbili kisiwani Zanzibar leo.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova (wa pili kulia), akiangalia jumba la Bait El Ajaib, Forodhani ambalo liliporomoka na sasa linafanyiwa ukarabati ndani ya Mji Mkongwe, ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya siku mbili kisiwani Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova (kulia), akipata maelezo ya vifaa alivyokuwa akitumia Mfalme Said Bin Sultan kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho, Dk. Amina Ameir Issa  baada ya kutembelea jumba la Wananchi, Forodhani, mjini Unguja, ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya siku mbili visiwani Zanzibar leo. 

No comments:

Post a Comment