Kaimu Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Regina Kikuli akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo, wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa kutoka kwa wadau wa afya wa Australia.
Muuguzi
Mkuu wa Idara ya Afya kutoka Serikali ya Australia, Bi. Catherine Stoddart
(kushoto), akimkabidhi funguo za magari ya kubebea wagonjwa, Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi.Regina Kikuli katika viwanja vya wizara
hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Magari hayo 2 yaliyotolewa kwa msaada wa wadau wa
afya wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Austaralia yatapelekwa kusaidia utoaji
wa huduma za afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe, Mkoani Pwani.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Regina Kikuli (kulia), akiwaonesha
waandishi wa habari (hawapo pichani), funguo za magari mawili ya kubebea wagonjwa
aliyokabidhiwa na wadau wa mashirika yasiyo ya serikali kutoka
Austaralia.
Wawakilishi wa wadau wa afya kutoka mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Austaralia, wakiongozwa na Muuguzi Mkuu wa Idara ya Afya ya Serikali ya Australia Magharibi, Bi. Catherine Stoddart (wa pili kutoka kushoto waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, mara baada ya kukabidhi msaada wa magari 2 ya kubebea wagonjwa. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
No comments:
Post a Comment