Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari bandarini jijini Dar es salaam leo jioni, wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa malori 26 kinyemela bandarini. Watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na Maofisa mbalimbali wa jeshi la Polisi na Bandari baada ya kukagua magari hayo, yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini hapo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe akikagua malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na kampuni ya Dhandho. Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Andrew Masaga, anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutaka kutoa malori hayo, akijitetea mbele ya Waziri (hayupo pichani), katika sakata hilo leo jinoni. Kushoto ni Mkuu wa Polisi Bandarini, Afande FM Misilimu.
Ofisa Utawala wa Kampuni ya Dhandho, Antipasi Otieno (kulia), akitoa maelezo mbele ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, kuhusu sakata hilo.
Mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo, ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kawaida katika idara yake.
Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.
No comments:
Post a Comment