Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Massawe alipomtembelea ofisini kwake leo, mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa Vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu, Fabian Massawe (kushoto), akimsomea taarifa fupi ya mkoa wake, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia), alipomtembelea ofisini kwake leo, mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yuko mkoani Kagera kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa Maendeleoa ya Vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akiongea na viongozi wa Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) leo, mjini Bukoba jinsi Serikali inavyoangalia uwezekano wa kuongeza mkopo kwa SACCOS zinazolenga shughuli za maendeleo ya Vijana kutoka shilingi milioni tano, hadi kumi kutokana na mahitaji ya fedha hizo kuwa makubwa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kagera, wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (hayupo pichani), wakati akiongea nao, kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia vijana kwa ukaribu katika Kata na kuweza kuwafundisha na kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo)
No comments:
Post a Comment