TANGAZO


Thursday, December 27, 2012

Diamond, Dimpoz wapagawisha usiku wa X-Mas Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam

 



Diamond akifanya manjonjo yake wakati alipopanda jukwaani kutumbuiza katika onesho la pamoja na Dimpozi kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam jana katika onesho la kusherehekea Sikukuu ya X-Mas.
 


Mashabiki kibao, kilammoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond wakati alipokuwa akitumbuiza ukumbini humo.
 


Hapa mzuka umepanda, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akishirikiana na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
 


Msanii Ommy Dimpoz, akiwa kwenye jukwaa, akifanya vitu vyake ukumbini humo.
 


Dimpoz na wasanii wake, wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
 


Omy Dimpoz, akipagawisha umati wa mashabiki waliofurika ukumbini humo, huku wakiripuka kwa mayowe ya furaha.
 


Platnumz akiwa hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake katika onesho hilo.
 


Diamond akipata kinywaji kwa ajili ya kupandisha mzuka kamili kwenye onesho hilo.
 


...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa hapa.


Msanii Juma Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki wake.
 
.
..Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
 


Vannesa Mdee, akipelekeshana puta na Dimpoz stejini, wakati wa onesho hilo.
 


KR Muller, akigonga mvinyo ndani ya mask.
 


Mbunge Zitto akiwa kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali wa kupasua.
 


Kikosi cha Diamond Platnumz kikiwa kazini katika onesho hilo.
 


Dimpoz na Vannesa Mdee, wakimwaga nyuki katika steji ya kupandisha na kushusha.
 


Angalia manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
 


Diamond akiwachizisha mashabiki wake katika onesho hilo.
 
.

Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao, hapa wakiwa wamemrusha juu mwenzao katika shoo yao ukumbini hapo.
 


Madansa hao, hapa wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki ukumbini humo.
 


Mbunge Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti chake baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
 


Platnumz na dansa wake kama 'The Wacko Jacko', wakiwa kazini.
 


Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake, ukumbini humo.
 


...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo alivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu, aliyeko mbele yake.
 


Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa ya akina Mbunge Zitto Kabwe (kushot0), ambaye ana onesha meno yote 32.
 


Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi (wa tatu kushoto), katika onesho hilo.
 


Prodyuza na mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini hapo.
 


...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaa!" Diamond akiimba wimbo wake maarufu huku akiwashirikisha mashabiki wake.
 


Madansa wa Extra Bongo, wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live, wakati wa onesho hilo.
 


Pozi la Platnumz, 'Diamond' wakati wa onesho lake hilo.
---
WASANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz', usiku wa kuamkia leo wameweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. (Picha zote na Richard Bukos na Issa Mnally/GPL)


 

No comments:

Post a Comment