Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakalalo kiliopo kijiji cha Kitigiri wilayani Geita, Gideon Msabila (kushoto), ambaye alimuelezea jinsi walivyonufaika na mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, fedha ambazo zimewawezesha kufungua duka la rejareja la bidhaa za nyumbani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia), akiangalia nguo zinazoshonwa na kikundi cha ushonaji kilichopo kijiji cha Bugalama, wilayani Geita, ambacho kimenufaika na mkopo wa shilingi milioni mbili, kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Halmashauri hiyo. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana, ili kuona fedha za mkopo zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha.
Vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka katika kijiji cha Kitigiri, wakifurahia fedha sh. 50,000/- walizopewa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wanne kushoto, aliyefichika), kwa ajili ya kununulia soda za Sikukuu ya Krismas. Waziri Dk. Mukangara aliwahimiza vijana hao, kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wanne kulia), akiongea jana na vijana wa kikundi cha kusaidiana kulima cha Busaka, kilichopo kijiji cha Kitigiri, wilayani Geita, umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi vya maendeleo vya kilimo ili weweze kupata mkopo wa kununulia pembejeo na kuweza kuzalisha chakula kwa wingi zaidi .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wanne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Geita, Kata ya Bukondo na kijiji cha Kitigiri, mara baada ya kumaliza ziara yake katika kijiji hicho jana, ili kuona fedha za mkopo za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, zimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda kilichopo kijiji cha Bugalama wilayani Geita, Enos Komanya, wakati alipotembelea kikundi hicho, ambacho kilipata mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Halmashauri. Waziri Dk. Mukangara alitembelea kijiji hicho jana, ili kuona fedha za mkopo zilizotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, zimewasaidiaje vijana kujikwamua kimaisha. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo)
No comments:
Post a Comment