TANGAZO


Tuesday, December 25, 2012

Wakristu waadhimisha siku ya Krismasi

 
Papa Mtakatifu Benedict
Papa Mtakatifu Benedict akiongoza misa ya Krismasi.
 
Wakristo kote duniani hii leo wanaadhimisha siku kuu ya Krismasi, siku ambayo wanakumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristu mjini Bethlehem.
Mjini Bethlehem kwenyewe, wakaazi wa mji huo waliadhimisha siku hiyo katika kanisa na Nativity lililojengwa miaka elfu moja mia saba iliyopita, eneo ambalo linaaminika ndiko Yesu alikozaliwa.
 
Mjini Vatican, Papa Mtakatifu Benedict XVI, aliongoza ibada ya Krismasi katika kanisa la St Peter's Basilica.
Akiongea wakati wa Ibada hiyo papa alitoa wito kwa Wakristo kumrejela Mungu.
Aliwaombia raia wa Israel na Palestina ili waweze kuishi kwa amani.

Raia wakiadhimisha Krismasi
Raia wa Viena wakiadhimisha Krismasi.
 
Vile vile papa Benedict aliwaombea raia wa Lebanon, Syria na Iraq.

Misa hiyo ambao kila mwaka huadhimisha saa sita za usiku iliadhimisha saa mbili mapema ili kumruhusu papa Benedict mwenye umri wa miaka 85 kumpunzika.

Baadaye hii leo,papa Benedikto atatoa ujumbe wake na baraka, unaojulikana kama Urbi et Orbi, kwa mji wa Roma na kwa Ulimwengu, kutoka kwa roshani ya St Peter's mjini Roma.

Mjini Bethlehem, kiongozi wa kanisa la katoliki pia aliwaomba raia wa Palestina na kusema wazi kuwa anaunga mkono kubuniwa kwa taifa huru la Wapalestina.

Fouad Twal alisema Krismasi hii itakuwa sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu na pia kuzaliwa kwa taifa jipya la Palestina.

Wakristu wakiadhimisha Krismasi
Wakristu wakiadhimisha Krismasi.
 
Hata hivyo alionya kuwa harakati za kaufikiwa kwa taifa huru la Palestina bado hazijamalizika na itahitaji ushirikiana zaidi.

Askofu huyo ambaye alizaliwa nchini Jordan aliongoza maandamana kutoka mji wa kale wa Jerusalem hadi ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, kupitia vizuizi vinavyogawanya mataifa ya Palestina an Israel na kituo cha ukaguzi kilichojengwa na serikali ya Israel.

Barani Afrika Wakirstu wa madhebu mbali walifurika katika makanisa mbali mbali kusherehekea siku kuu ya Krismasi.

Hata hivyo, mjini Nairobi, Wakenya wengi ambao walitaka kusafiri kujiunga na jamaa zao katika sehemu za mashambani, wamekwama katika vituo mbali mbali vya basi kutokana na ukosefu na mabasi ya kutosha na pia kupandishwa kwa nauli.

Kampuni nyingi za mabasi zimeongeza nauli kutokana na idadi kubwa ya abiria.

No comments:

Post a Comment