TANGAZO


Tuesday, December 25, 2012

Watu watano wauawa Nigeria

 

Watu wakisimama mbele ya Kanisa
Picha ya watu waliosimama mbele ya Kanisa Katoliki lililoshambuliwa nchini Nigeria, Desemba 25,2011.
 
Majeshi ya usalama kaskazini mwa Nigeria wamesema watu wenye silaha wamekishambulia kijiji kimoja chenye wakaazi wengi Wakristo na kuua watu watano na wengine wanne kujeruhiwa.
 
Msemaji wa jeshi ameiambia BBC kuwa washambuliaji waliwafyatulia risasi waumini wakiwa Kanisani katika ibada ya mkesha wa Krismasi.

Amesema mtuhumiwa mmoja wa mashambulio hayo amekamatwa, na ulinzi katika eneo hilo umeimarishwa ili kuwahakikishia usalama wakaazi wa eneo hilo.

Msemaji huyo amesema nyumba kadha karibu na kanisa lililoshambuliwa zilitiwa moto.

Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na mashambulio hayo katika jimbo la Yobe, lakini katika siku za nyuma kikundi cha Kiislam cha Boko Haram kiliwashambulia Wakristo katika jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment