TANGAZO


Tuesday, December 25, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal azuru kaburi la Rais Abdulwakil, Makunduchi, amtembelea mwasisi wa Afro-Shiraz, mzee Ali Khamis


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), akiwa mbele ya kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar, marehemu Idris Abdulwakil, wakati alipozuru Kijiji cha Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja jana. Rais Abdulwakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk. Bilal alifika eneo hilo   akiwa katika ziara ya kuwatembelea wazee mbalimbali mkoani humo, Desemba 24, 2012. (Picha zote na OMR)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Makunduchi, wakati alipokuwa akitoka kuzuru kaburi la Rais wa zamani wa Zanzibar, marehemu Idris Abdulwakil Nombe, Mkoa wa Kusini Unguja. Rais Abdulwakil alifariki dunia mwaka 2001. Dk. Bilal alifika eneo hilo, akiwa katika ziara ya kuwatembelea wazee mbalimbali mkoani humo jana, Desemba 24, 2012. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mzee Ali Khamis Abdallah (98), ambaye ni mmoja kati waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha Vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee leo, Desemba 25, 2012, nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja. Kulia ni mke wa mzee Ali, Asha Ali Ghulam Hussein.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Ali Khamis Abdallah (98) ambaye ni mmoja kati waasisi 10, waliokaa pamoja na kuunganisha Vyama vya African Association na Shiraz Association na kuwa Chama cha Afro Shiraz Party (ASP), wakati akiwa katika ziara yake ya kutembelea wazee leo, Desemba 25, 2012, nyumbani kwake Mbweni, mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment