TANGAZO


Tuesday, December 25, 2012

Wafanyakazi wa Exim Bank, tawi la Morogoro watoa msaada kwa watoto yatima

Meneja wa Benki ya Exim ya Tanzania Tawi la Morogoro, Anna Wesiwasi (kulia), akikabidhi katoni ya juisi kama sehemu ya msaada wa vyakula mbalimbali uliotolewa na benki hiyo kwa Yatima wa kituo cha Mary Sisters cha Morogoro - Mgolole leo, wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea kituo hicho katika kusherehekea Sikukuu ya Christmas na watoto hao. Benki hiyo ilitoa mchele kilo 50, sukari kilo 25, unga wa ngano kilo 25, mbuzi mmoja, mafuta ya kula lita 10, katoni mbili za juisi na boksi moja la biskuti. Kwa mujibu wa Bi. Wesiwasi, wafanyakazi wa benki hiyo, wametembelea kituo hicho kwa ajili ya kujumuika na yatima hao katika kusherehekea Sikukuu ya Christmas. (Na Mpiga Picha Wetu)

 Meneja wa Benki ya Exim ya Tanzania, Tawi la Morogoro,  Anna Wesiwasi (kulia), akizungumza jambo na yatima wa kituo cha Mary Sisters cha Morogoro - Mgolole leo, wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea kituo hicho, kusherehekea Sikukuu ya Christmas na watoto hao. Benki hiyo ilitoa mchele kilo 50, sukari kilo 25, unga wa ngano kilo 25, mbuzi mmoja, mafuta ya kula lita 10, katoni mbili za juisi na boksi moja la biskuti. Kwa mujibu wa Bi. Wesiwasi, wafanyakazi wa benki hiyo, wametembelea kituo hicho kwa ajili ya kujumuika na yatima hao katika kusherehekea Sikukuu ya Christmas. 

Mmoja kati ya wafanyakazi wa Benki ya Exim ya Tanzania, tawi la Morogoro, akimpeleka mbuzi aliyetolewa na benki hiyo kwa ajili ya kumchinja wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea kituo cha Mary Sisters cha Morogoro - Mgolole leo, kusherehekea Sikukuu ya Christmas na watoto hao. Benki hiyo ilitoa mchele kilo 50, sukari kilo 25, unga wa ngano kilo 25, Mbuzi mmoja, mafuta ya kula lita 10, katoni mbili za juisi na boksi moja la biskuti.

Meneja wa Benki ya Exim ya Tanzania Tawi la Morogoro, Anna Wesiwasi (wa pili kulia, mstari wa nyuma), akiwa katika picha ya pamoja na mama mlezi wa kituo cha Mary Sisters cha Morogoro – Mgolole (wa tatu kulia),  na Mkuu wa kituo hicho, Sister Felister Mwinuka (kulia), pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Exim na baadhi ya watoto yatima wa kituo hicho, mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa watoto hao, wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipotembelea kituo hicho, kusherehekea Sikukuu ya Christmas na watoto hao. Benki hiyo ilitoa mchele kilo 50, sukari kilo 25, unga wa ngano kilo 25, Mbuzi mmoja, mafuta ya kula lita 10, katoni mbili za juisi na boksi moja la biskuti.

No comments:

Post a Comment