TANGAZO


Saturday, December 8, 2012

WAMA watoa vitanda 80 kwa Hospitali ya Muhimbili

 
Mwenyekiti wa WAMA, mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vitanda 80 kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela.
 
Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi vitanda 80 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akisoma hotuba yake, wakati wa hafla hiyo.
 
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (MNH), Dk. Marina Njelekela akimshukuru mama Salma Kikwete mara baada ya kupokea msaada wa vitanda hivyo leo.
 
Baadhi ya Wganga na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakishuhudia tukio hilo.
 
Mama Salma Kikwete akiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Marina Njelekela (kushoto), wakati akielekea wodini kuwatembelea wagonjwa. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
 
Mama Salma Kikwete, akimjulia hali Anna Razalo kutoka Nyegezi Mwanza mmoja wa wagonjwa wa moyo aliyelazwa hospitalini hapo. (Picha zote kwa hisani ya Fullshangwe blog)

No comments:

Post a Comment