Mkurugenzi Mtendaji wa
Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki (EABC), Andrew Luzze Kaggwa,
akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja.
Mafunzo hayo yanahusisha waandishi wa habari kutoka nchi zote wanachama wa
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa,
akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu
wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja.
Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa Baraza la Asasi
za Kijamii la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha, akizungumza katika
mafunzo hayo, juu ya ushiriki wa Asasi za kiraia katika uelimishaji na ufikishaji
wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa Siasa za
Afrika ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu,
akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati la ufundi nalo wakati wote lilikuwa katika
wakati mgumu wa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Kutoka kushoto ni Aline
Ellermann, Elizabeth Wanyoike na Hussein Karim wote kutoka ofisi ya GIZ, ambao
ndio wawezeshaji mafunzo hayo yaliyoandaliwa pamoja na EABC.
Kuna wakati mambo
yanaonekana hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike (kulia), akikuna
kichwa, huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona Mbabazi kutoka Rwanda akimshukuru Ofisa
Mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa kwa maelezo juu ya Baraza hilo. Kati ni Jenerali
Ulimwengu na Aline Ellermann.
Bizimana Jean-Marie akitoa zawadi kwa Dk. Martin
Mwadha wa Asasi za Kiraia za EAC. Wengine pichani kutoka kushoto ni Elizabeth
Wanyoike wa GIZ, Balozi Jeremy Ndayiziga, Andrew Kaagwa na Jenerali
Ulimwengu. (Picha zote kwa hisani ya Father Kidevu Blog)
No comments:
Post a Comment