Mwamuzi wa pambano la masumbwi, Said Chaku (katikati)
akimwinua mkono juu bondia Obete Ameme, baada ya kumtwanga mpinzani wake katika
raundi ya kwanza kwa K,O katika pambano lao lililofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Na
Mwandishi wetu, Bagamoyo
MASHABIKI na
wapenzi wa mchezo wa masumbwi, waishio Wilaya ya Bagamoyo, wamewataka viongozi
wa mchezo huo kutopendelea kufanya mashindano ya mchezo huo jijini Dar es
Salaam, pekee na badala yake wapeleke mchezo huo wilayani
humo.
Wakizungumza na mtadao huu
baada ya kumalizika kwa pambano la ngumi, katika ya Zumbe
Kikuru, na Toma Kato, mashabiki hao walisema kuwa wanahamasika sana na mchezo
huo, lakini hawapati fulsa ya kuuona mara kwa mara kutokana na wilaya yao
kusahaulika na waandaaji wa mchezo huo.
Aidha walisema kuwa waandaaji
wengi wamekuwa wakisita kupeleka mapambano ya ngumi wilayani humo, kwa kudhani
mchezo huo hauna mashabiki wa kutosha mjini Bagamoyo, jambo ambalo si la
kweli.
''Hebu ona mashabiki waliojitokeza leo kushuhudia mchezo huu, hawa
wote ni mashabiki wa kweli ila wanakosa burudani hii kutokana na kulazimika mara
kwa mara kusafiri hadi jijini dar kwa ajili ya kushuhudia mchezo huu, tunawaomba
sana viongozi wa vyama vya mchezo wa ngumi watukumbuke na sisi kwa kutuletea
angalao mara moja kwa miezi miwili hivi mapambano'' alisema shabiki mmoja
aliyejitambulisha kwa jiana na Said Bubelwa |
No comments:
Post a Comment