TANGAZO


Monday, December 3, 2012

TBL yadhamini Siku ya Ukimwi duniani, Watu 400 wajitokeza kupima ukimwi kwa hiyari


 

Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha wakiwasha mshumaa na Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, wakati wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiadhimisha Siku ya Ukimwi duniani, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto. Zaidi ya watu 400 walipima Virusi vya Ukimwi kwa hiyari katika kuadhimisha siku hiyo.
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha pamoja na Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Orio wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, Dar es Salaam.
Banda lililowekwa na TBL katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam kwa ajili ya wafanyabiashara kushiriki kupimwa virusi vya Ukimwi kwa hiyari.
Mkazi wa Ilala Mchikichini, Abdalah Lukali (58), kushoto, akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, tayari kupimwa virusi vya Ukimwi katika banda lililowekwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
Fundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Shabani Kilango (kushoto), akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, Elizabeth Sangu tayari kupimwa virusi vya Ukimwi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, wakiadhimisha ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam juzi.
Mtalaamu wa upishi wa TBL, Edward Mvula akichukuliwa damu tayari kupimwa virusi vya Ukimwi
Wafanyakazi wa TBL, wakinunua keki ambazo makusanyo yake walipatiwa watoto wanaoishi na virusi vya Ukimwi wa Kituo cha Tocha+
Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (kulia) akiwauziwa keki hizo, viongozi wa Kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin

Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto.

Wasanii wa Tocha+ wakilia kwa uchungu walipokuwa wakiigiza igizo la UKIMWI na kugundua wote wameambukizwa kwa kutembea na Baba mwenye nyumba. Kutoka kushoto ni Ruth Ngwembele, Gift Andrew na Emma Julius.
Wasanii wa Kikundi cha Tocha+, Fadhili Malidodi (kushoto) na Richard Kessy wakilia wakati wakiigiza igizo la UKIMWI wakati wa maadhimisho hayo.
Dk. Mwaikasu (wa pili kushoto), akimkabidhi Henry Ramadhan vyombo vya muziki baada ya kuwa mmoja wa washindi wa droo iliyochezeshwa kwa waliopima virusi siku hiyo.
Leonald Mitoris (kulia) wa Idara ya Uhandisi TBL, Akipatiwa zawadi y jiko la gesi.
Meneja wa Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam, Calvin Martine akimpatia zawadi ya jiko la gesi Josephat Magesa ambaye alikuwa miongoni mwa washindi waliopima virusu vya ukimwi kwa hiyari.

Yolanda Minja (kulia), akipata zawadi ya jiko la gesi
Julius Matola (kulia) wa Idara ya Mauzo wa TBL, akipatiwa zawadi ya simu
Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo akimpatia zawadi ya simu Abubakar Mambo
Timu ya TBL iliyoandaa maadhimisho hayo.(Picha zote na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio blog)

No comments:

Post a Comment