Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo,
Julius Kihampa akimvisha pete ya ndoa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1),
Grace Kingarame wakati wa kufunga pingu za maisha kwenye Kanisa la Anglikana la
St. Albano Dar es Salaam jana.
Julius Kihampa akimvisha pete mkewe, Grace Kingarame mbele ya Padrii Cosmas Mhina.
Kihampa akiwa na mkewe Grace Kingarame
Ibada ya kuwafungisha ndoa ikiendelea
Kihampa akimvua shela mkewe Grace
Kihampa akila kiapo cha uaminifu katika ndoa mbele
ya mkewe Grace. Kulia ni Patroni wake Chacha Maginga na Matroni Levina.
Grace Kingarame akila kiapo
cha uaminifu katika ndoa mbele ya mumewe Kihampa na kanisa.
Padri Cosmas Mhina akiwafungisha ndoa Kihampa na
Grace
Kwaya ya kanisala hilo ikitumbuiza
Baadhi ya ndugu,
jamaa na marafiki wakishuhudia ndoa hiyo ikifungwa
Baadhi
ya wapambe wa harusi hiyo wakiwa kanisani
Padri
akiwaelekeza jinsi ya kuweka saini hati ya ndoa
Kihampa
na Grace wakikabidhiwa hati za ndoa huku wakimwaga tabasamu la nguvu.
Wanandoa hao
wakiwa na furaha huku wakionesha hati zao za ndoa
Bwana harusi Julius Kihampa akiwa amejiinamia
akitafakari jinsi ya kukabiliana na maisha mapya ya ndoa
Maharusi
wakitoka kanisani baada ya kufunga ndoa
Kweli wanameremeta
Maharusi
wakipanda kwenye Lemousine lililoandaliwa kwa ajili yao
Msafara wa maharusi hao ukiondoka kanisani
kuelekea Coco Beach. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)
No comments:
Post a Comment