Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (kushoto), akikabidhiwa tuzo yake ya ufanyakazi bora wa kitengo na Waziri wa wizara hiyo, Dk. William Mgimwa katiaka tafrija iliyofanyika jana wizarani hapo.
Mkuu wa Mfuko wa Mikopo wa Hazina kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Christina Ngonyani, akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (kulia), katika tafrija fupi ilifanyika jana jijini Dar es Salaam kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa mfanyakazi bora kwa mwaka 2012.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah (kushoto), akipongezwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. William Mgimwa (kulia), baada ya kuwa mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara kwa mwaka 2012, wakati wa hafla fupi ya kuwapa tuzo wafanyakazi hao, iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (katikati), akizungumza wakati alipokuwa akiwapongeza wafanyakazi bora wa Wizara ya Fedha waliochaguliwa mwezi Mei mwaka huu kuwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012 wakati wa tafrija fupi ya kuwazawadia ilifanyika jana mjini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment