Nohodha wa timu ya Netbal ya Bunge, Grace Kiwelu. (Picha zote na Mwaibale.blogspot) |
Wabunge wakiwa na kombo la Ubingwa wa Netbal walililolipata katika mashindano ya Bunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijijni Nairobi nchini Kenya. |
Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na kombo la Ubingwa wa Netbal walililolipata katika mashindano ya Bunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijijni Nairobi nchini Kenya. |
Wabunge wakiwa na kombo hilo la Ubingwa wa Netbal walililolipata katika mashindano ya Bunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijijni Nairobi nchini Kenya. |
Na Dotto Mwaibale
TIMU ya Bunge la Tanzania imerejea nchini na kombe baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa netiboli kwenye mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki yaliyofikia tamati mwishoni mwa wiki Nairobi Kenya.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam , Mwenyekiti wa timu hiyo Mbunge wa Kinondoni Idd Azani amesema wanajivunia ushindi huo.
"Tunajivunia ushindi huu mkubwa tuliopata kwa mchezo huo uliochezwa na wabunge wenzetu kwani katipa mpira wa miguu kulikuwa na changamoto kwa upande wa wenzetu kuchezesha mamluki" alisema Azan.
Alisema katika mpira wa miguu walifanikiwa kupata nafasi ya tatu baada ya kuibwaga Rwanda kwa mabao 5-0 ambapo pia waliondolewa baada ya kuingia nusu fainali na timu ya bunge la Afrika Mashariki.
Alisema katika mashindano hayo walishinda mechi tatu kwa kuifunga Rwanda mabao 5-0 kwa awamu ya kwanza na katika awamu ya pili waliifunga tena Rwanda kwa mabao 6-1.
Alisema changamoto katika mashindano hayo ni kushirikishwa mamluki wanne kwenye mpira wa miguu jambo ambalo waliliwasilisha kwa wahusika.
Alisema mashindano hayo yenye lengo la kuimarisha mshikamano kwa wabunge wa Afrika Mashariki yalianza kufanyika mwaka 2009 kwa kuzishirikisha timu 5 za Rwanda, Uganda, Bunge la Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania.

No comments:
Post a Comment