Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kushoto), akiwa na Diwani wa Ludewa Mpambalyoto wakila kiapo, wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula.
Viongozi wa CCM, Mkoa wa Njombe, wakishirikiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula (wa pili kulia), kuwaongoza wanachama wapya wa CCM, zaidi ya 600 waliojiunga na cahama hicho leo, wakati wa mapokezi ya makamu huyo. Wa kwanza kuli ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini, ambaye pia ni Spika wa Bunge, Anne Makinda, wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Njombe, Deo Sanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini na anayefuatia ni Katibu wa CCM, mkoani humo, Hosea Mpangike.
Wananchi pamoja na wanachama wa CCM, Mkoa wa Njombe, wakishiriki kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Phili Mangula, mkoani humo leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula akishuka jukwaaani baada ya kukabidhiwa zana za kijadi na wazee wa Mkoa wa Njombe kama nyenzo za kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya Chama. Mangula alikabidhiwa zana hizo katika mkutano wa mapokezi, uliofanyika mjini Njombe.
Mangula akiwa amebeba zawdi alizopewa na wazee Njombe
Mangula akikabidhiwa vitendea kazi na mzee wa Njombe
Umati wa wananchi waliofika kumpokea
Baadhi ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakionesha kuunga mkono hotuba zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula.
Kiongozi wa dini akimuombea na kumpa maneno ya hekima, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula.
Mangula na Spika Makinda wakiwa wameinamisha vichwa wakati wa maaombi maalum kutoka madhehebu yote ya dini mkoani Njombe leo.
Kiapo kwa wanachama wapya wa CCM
Mapokezi ya Mangula Njombe yatisha
Wapanda pikipiki wakiongoza msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, wakati wa mapokezi yake, mkoani Njombe leo. (Picha zote na Francis Godwin)
Na Francis Godwin, Njombe
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe amewakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini, linaloongozwa na mbunge wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga, kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini, mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula.
Filikunjombe ambaye alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo, mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe, alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya Serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.
Hivyo alisema kuwa imani ya wana CCM kwa safu ya sasa chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Abdalaman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa bara Mangula na Makamu wake wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine ndani ya Chama ni matumaini mapya kwa wana CCM na tishio kwa vyama vya upinzani.
" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .
Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.
Kwa Upande wake Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.
" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"
Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.
Aidha amehimiza nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.
Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo.
Mangula alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa Katika katika utawala bora na kufanya mambo mengi zaidi ya kimaendeleo na iwapo wapo watu wanaosema CCM haijafanya lolote toka ilipoingia madarakani wanakionea Chama kwani maendeleo ambayo jamii inanufaika nayo sasa ni matunda ya CCM.
Awataka Vijana kupunguza jazba kwa kuwa kukubali kutumikishwa na watu wasiopenda amani ili kuvuruga amani kuwa iwapo vijana watashindwa kuepuka kutumika kwa kuvuruga amani Taifa litakwenda pabaya.
Akimkaribisha Mangula Mkoani Njombe Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga alisema kuwa CCM mkoani Njombe kimeendelea kutekeleza vema ilani ya uchaguzi pamoja na kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Sang a alisema kuwa katika mji wa Makambako CCM iliahidi maji, huduma za Afya kwa maana ya kuwa na Hospitali ya wilaya pamoja na kuwawezesha wananchi wa pembezoni kuwa na huduma ya umeme na zoezi hilo linaendelea na tayari naibu waziri wa nishati na Madini amepata kufika mjini Makambako Jana na kutembelea mradi huo.
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike alisema kuwa mbali ya wanachama wapya zaidi ya 1000 kujiunga na Chama hicho ila lipo kindi kubwa la wapinzani Kutoka Chadema ambao wanataka kujiunga na CCM ila wanaandaliwa mpango maalum wa kupokelewa.
No comments:
Post a Comment