TANGAZO


Sunday, December 16, 2012

Koffi Olomide alivyopagawisha Leaders Club


Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide, akiwaongoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa, wakati wa onesho lake la 'Usiku wa Tusker Carnival', lililofanyika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, ambapo pia alisindikizwa na bendi za Sky Light, Twanga Pepeta, Diamond Sound na Mapacha watatu.
Koffi Olomide na mwimbaji wake, Cindy (kushoto), wakiwaongoza wanenguaji kushambulia jukwaa, wakati wa onesho la 'Usiku wa Tusker Carnival', lililofanyika Viwanja vya Leaders Club, usiku wa kuamkia leo.
 Wanenguaji wa Koffi Olomide, wakishambulia jukwaa katika onesho hilo.
 Wanenguaji wakilishambulia jukwa, viwanja vya Leaders.
Koffi Olomide, akiimba jukwaani, baada ya kupanda na kushangiliwa na umati mkubwa mashabiki waliojitokeza kushuhudia onesho hilo, usiku wa kuamkia leo, Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wanenguaji wa Koffi, wakiingia kwenye jengo waliloandaliwa rasmi kufikia kabla ya kupanda jukwaani, ndani ya Viwanja vya Leaders.
Koffi, akiwasili katika eneo aliloandaliwa kupumzika kabla ya kupanda jukwaani kwa onesho.
Koffi, akiteta jambo na Boss wa Tusker, baada ya kuwasili viwanjani hapo kwa onesho.
Koffi, akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SLB), watengenezaji wa Bia ya Tusker, iliyoandaa onyesho hilo, kabla ya kuanza onesho lililowapagawisha mashabiki viwanjani hapo.
Wanenguaji wa Koffi, wakiwa wamepumzika wakisubiri kupanda jukwaani kwa onesho baada ya kuwasili viwanjani hapo.
Boss wa Tusker na wafanyakazi wa Kapuni hiyo, wakipozi kusubiri kumpokea Koffi kabla ya kuwasili kwenye viwanja hivyo kwa onesho hilo.
Wadau, waandishi wa habari, nao walikuwepo uwanjani hapo kushuhudia onesho hilo, ambalo mbali na mwanamuziki wa Kimataifa wa DRC, Koffi Olomide, bendi kadhaa za nyumbani nazo zilitumbuiza katika tamasha hilo.
Sehemu ya mashabiki wa muziki wa dansi, wakifurahia ladha ya muziki wa Koffi.
Waimbaji wa bendi ya Sky Ligth, Jonico Flower Maua Gwa, akipozi na wanenguaji wake na mwanamuziki mwenzake, Kushaba.
Asha Baraka (kushoto), Macheni na baadhi ya wadau wa muziki wa dansi wakifuatilia onyesho hilo.
Mshereheshaji wa onesho hilo, ambaye pia ni mtangazaji wa TBC1,  Ben Kinyaiya, akisebeneka tar tiiiiibu.....
Hapa sebene la wana wa Koffi, lilikolea kiasi cha kuwafanya mabosi hawa wa Tusker kushindwa kuvumilia na kuamua kuanza kuzirudi.
Sehemu ya mapaparazi waliokuwapo wakichukua picha za matukio ya onesho hilo jukwaani.
 Akinadada warembo nao pia walikuwepo kushuhudia onesho hilo.
 Sehemu ya mashabiki wakishiriki kucheza muziki wa Koffi Olomide, wakati wa onesho hilo.
Koffi, akimpongeza Mkurugenzi wa Clouds, Joseph Kusaga (katikati) kwa kufanikisha onesho hilo.
Paparazi wa magazeti ya Ijumaa na Uwazi, akisikitika haikuweza kufahamika mapema alikuwa akisikitika aidha kamera yake kushindwa kufanya kazi ama kukosa tukio katika onesho hilo.
Hapa mabosi wa Serengeti Breweries wakifurahia jambo kwenye onesho hilo. (Picha zote na mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment