TANGAZO


Friday, December 14, 2012

Rais Kikwete azindua rasmi mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Temeke jijini Dar es Salaam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 290 za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), maeneo ya Kibada, Kigamboni, Wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam jana, December 13, 2012. Kushoto ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye (kulia), anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita na Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu,
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea moja ya nyumba za NHC za mradi wa Kibada, baada ya kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 290 za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), maeneo ya Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam jana, December 13, 2012. Wa tatu kulia ni Mama Salma Kikwete, wa pili kushoto ni  Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe  kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 290 za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) maeneo ya Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam jana, December 13, 2012, akiwa pamoja na Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye Naibu Waziri wa Fedha, Sara Salum, Mwanaseheraia Mkuu wa Serikali. Jaji Frederick Werema, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita , Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu. (Picha zote na Ikulu)


No comments:

Post a Comment