Wapiga vyombo (magita) wa bendi hiyo, waking'uta vyombo hivyo, wakati bendi ilipokuwa ikitumbuza katika onesho hilo.
Mashabiki wa bendi hiyo, wakijimwaga stejini, baada ya kupandwa na mdadi wa midundo ya bendi hiyo.
Wacheza shoo wa bendi hiyo wakiwajibika stejini, kukonga nyoyo za mashabiki waliokuwa wamejazana ukumbini humo.
Wacheza shoo wa bendi hiyo wakitia madoido wakati walipokuwa wakiwajibika stejini kwenye onesho hilo.
Wacheza shoo wakionesha ufundi wao wa kuzirudi ngoma za kundi hilo, wakati walipokuwa wajibika stejini.
Wacheza shoo wa bendi hiyo, walitia fora sana katika onesho hilo, kwani ilikuwa kama vile waliopagawa kwa kutoa shoo za hali ya juu zilizowaacha mashabiki vinywa wazi.
Hizi ni baadhi tu ya majamboz ya wacheza shoo wa bendi hiyo, jinsi walivyokuwa wakiwajibika jukwaani na kuonesha thamani halisi ya kuwepo kwenye kundi hilo linalopiga muziki wenye asili ya Kizaire.
Sasa angali mwenyewe mambo ya shoo za vijana hao wa kazi wa kundi hilo, zilivyokwenda shule na kumvutia kila mtu aliyesogelea karibu na ukumbi huo katika onesho hilo.
Hii ni moja tu ya staili za shoo zilizokuwa zikipakuliwa na vijana wacheza shoo wa bendi hiyo, ukumbini humo.
No comments:
Post a Comment