TANGAZO


Sunday, December 9, 2012

Rais Kikwete aongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Ulinzi nchini, Dk. Jakaya Kikwete akiwasili kwa gari maalum la kijeshi na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara, leo Disemba 9, 2012, maadhimisho yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu, ikiwa ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.

 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalaama katika maadhimisho hayo.
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalaama katika maadhimisho hayo.
 
Kikosi cha Brass Band cha Jeshi la Ulinzi na Usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
 

Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo. Kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. Gharib Mohamed Bilal na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, mzee Ali Hassan Mwinyi.
 
Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam  leo katika maadhimisho hayo.
 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Joseph Kabila akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaa leo asubuhi kwa ajili ya maadhimisho hayo.
 
 
Mama Maria Nyerere, akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mizengo Pinda akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo, huku akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.
 
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, mzee Ali Hassan Mwinyi, akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
 
Vikosi vya Ulinzi na Usalama, vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.
 
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed Bilal, akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 
Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo, Disemba 9, 2012, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi.
 
Rais Dk. Jakaya Kikwete (kulia), akipokea gwaride la heshima la vikosi vya Jeshi la Ulinzi na Usalama, lilipokuwa likipita mbele yake. Wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Namibia, Ifikepunye Pohamba na mke wa Rais, mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo.
 
Vijana wa chipukizi wakionesha michezo na ujumbe mbalimbali, wakati wa maadhimisho hayo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo.
 
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika mfano wa silaha.
 

Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi  wa Tanzania (JWTZ), kikitoa heshima zake kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, jijini leo.
 
Kikosi cha ardhini cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Fullshangwe blog)
 

No comments:

Post a Comment