Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mantra Tanazania, Asa Mwaipopo (wapili kushoto), akibadilishana nyaraka za
makubaliano na Mkuu wa Kituo chaUshonaji cha 'Utete Tailoring Mart', kilichopo
Songea, Mkoani Ruvuma Athanas Nyumbi (katikati), wakati wa hafla ya kukabidhi
cherehani ya kisasa itakayotumika kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya
Mantra .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra
Tanazania, Asa Mwaipopo (kushoto) akikabidhi cherahani ya kisasa kwa Mkuu wa
Kituo chaUshonaji cha 'Utete Tailoring Mart', Athanas Nyumbi (kulia), ambayo itasaidia
kutengeneza sare za wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra
Tanazania, Asa Mwaipopo (wa pili kushoto), akionesha sare za wafanyakazi wa
Kampuni hiyo, zinazotengenezwa na Kituo chaUshonaji cha 'Utete Tailoring Mart',
kilicopo Songea, mkoani Ruvuma wakati wa hafla fupi ya kukabidhi cherahani ya
kisasa kwa Mkuu wa Kituo hicho Athanas Nyumbi (kushoto), mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya Mantra Tanazania Asa Mwaipopo (kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Ushonaji cha
'Utete Tailoring Mart', kilichopo Songe, mkoani Ruvuma Athanas Nyumbi (kulia), wakitia
sahihi hati za makubaliano zitakazowezesha kituo hicho, kutengeneza sare za
wafanyakazi wa Kampuni ya Mantra. (Picha zote na mpiga picha wetu)
Na mwandishi wetu ,
Songea
KAMPUNI ya Mantra Tanzania
imeendeleza jitihada zake za kusaidia jamii inayoizunguka kwa kutoa cherehani
yakisasa inayotumia mfumo wa komputa kwa Kituo cha Ushonaji cha Utete Tailoring
Mart kilichopo mjini Songea , Mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika hafla fupi
ya kukabidhi cherehani hiyo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mantra Tanzania Asa Mwaipopo alisema kuwa kampuni yake imejizatiti kusaida
kupunguza umasikini kwa kusaidia miradi mabali mbali ya maendeleo kwenye Mkoa
huo wa Ruvuma.
Mwaipopo alisema tayari
kampuni yake imesaini hati za makubaliano na Kituo cha Ushonaji cha Utete ambapo
kituo hicho kitatengeneza sare (uniform) za wafanyakazi wa kampuni yake hali
ambayo itasaidia kujenga uwezo wa kituo hicho.
“Kampuni ya Mantra ina nia
ya kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo kwakutambuma umhimu wa miradi hiyo
katika kupunguza umasikini. Kwa lengo hilo, leo tunakabidhi cherehani ya kisasa
kwa kituo hichi cha Utete na tunaamini jitihada zetu zitakuwa chachu ya
maendeleo ya kituo hiki.
Mwaipopo alisema cherehani
hiyo imetolewa kwa mtindo wa mkopo wa mzunguko (Revolving Fund) na kusema kuwa
pesa itakayopatikana itasaidia kuendeleza washonaji wengine mkoani
humo.
“Atalipia kwa utaratiu wa
kazi ambazo tutakuwa tukimpa kwa makato ya taratibu. Pesa ambayo itapatikana
itasaidia kuinua washoinaji wengine. Ni matumaini yangu kuwa cherehani hii
itatumika kwa matumizi sahihi iliiweze kuka muda mrefu ,” alisema
Mwaipopo.
Mwaipopo alisema kuwa Kampuni
yake inatakribani wafanyakazi 150 na kusema kuwa idadai hiyo itaongozeka
maradufu kufikia wafanyakazi 1500 kipindi Mradi wake wa Urani wa Mto Mkuju
utakapoanza.
“Ni matumaini yetu kuwa sare
za wafanyakazi wote hao zitatengenezwa na kituo hich cha Utete. Hii sikazi wa
mtu mmoja kwahiyo lazima kituo hiki kiaajiri washonaji wengine. Ni matumaini
yetu kuwa wananch watachangamkia fursa zitakazopatikana,” alisema.
Naye Mkuu wa Kituo hicho cha
ushonaji cha Utete Atnas Nyumbi alisema msaada huo umekuja muda muafaka na
kuahidi kutumia cherehani hiyo vizuri ilikupata mafanikio makubwa
zaidi.
“Tunashukuru Kampuni ya
Mantra kwa kuwa na imani na kituo chetu. Tunaahidi kutumia cherehani hii vizuri
ilituweze kupata mafanikio na kusonga mbele,” alisema Nyumbi.
Kampuni ya Mantra Tanzania
imekuwa mstari wa mbele katika kusadia miradi mbali mbali ya maendeleo kwenye
Mkoa wa Ruvuma ikwemo miradi ya afya, elimu, utunzaji wa mazingira pamoja na
michezo.
No comments:
Post a Comment