TANGAZO


Friday, December 7, 2012

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Charles Kitwanga ahitimisha ziara katika Viwanda na Mahoteli jijini na kukemea wanaochafua fukwe za bahari

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa tatu kulia) akiwasili katika Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha Shelys kilichopo Mwenge jijini Dar huku akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga na Wataalamu wa Kitengo cha Mazingira kutoka katika Wizara yake katika muendeleo wa ziara za kushtukiza Viwandani kukagua mfumo wa mazingira ya maji taka yenye kemikali katika viwanda hivyo kama unaendana na viwango vilivyowekwa.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akieleza dhumuni la ziara yake katika kiwanda hicho kwa Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha dawa cha Shelys Bw. Nissa Mwaipiana (kulia).
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwandani hapo Bi. Shemina Pera Somji akitoa maelezo kwa Naibu Waziri na Ujumbe wake.
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akimwongoza Mh. Charles Kitwanga kwenda kukagua sehemu ya kutibu maji taka yenye kemikali.
Mwendesha Mashine wa Kiwanda hicho Bw. Patrick Mapunda (mwenye koti) akitoa ufafanuzi Kwa Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga wa namna wanavyokusanya na kuyatibu maji taka yanayotokana na uzalishaji kiwanda hapo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maagizo wa NEMC baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho kutofikia ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga(wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden (kulia) kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho. Country PAC Manager wa kiwanda hicho Bw. Evans Mlewa (wa pili kushoto) na kurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden akitoa Maelezo kwa Mh. Kitwanga juu ya Mitambo Mipya ya Kisasa yenye kiwango cha Kimataifa kwa ajili ya kutibu maji taka katika Kiwanda hicho.
Mh. Kitwanga na Ujumbe wake ukitizama Bwawa la Samaki linalotumika kufanyia majaribio ya maji taka ambayo yamekwisha safishwa kwa ajili ya matumizi mengine kiwandani hapo.  (Picha zote na Fullshangwe blog)

No comments:

Post a Comment