TANGAZO


Monday, December 17, 2012

Meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi afurahishwa na gazeti la matangazo la Dar Metro linalogawiwa bure jijini

 


Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi (kushoto), akikabidhiwa gazeti jipya la Dar Metro na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee, Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi (kushoto), akisoma gazeti jipya la Dar Metro alilopelekewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, inayochapisha gazeti hilo, Juma Pinto (kulia), ofisini kwake Karimjee, Dar es Salaam leo. Gazeti hilo maalumu kwa matangazo linalotolewa mara mbili kwa mwezi, hugawiwa bure kwa wasomaji. Kampuni hiyo, huchapisha pia magazeti ya Jambo Leo, jarida la Jambo Brand Tanzania na Staa Spoti.

Meya Massaburi akilipitia vizuri gazeti hilo, litakalokuwa linaandikwa kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Pinto akimwelezea jambo Meya Massaburi, alipofika ofisini kwake, Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment