TANGAZO


Monday, December 17, 2012

Aliyedhaniwa kufa kwenye ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi afunga ndoa, Hakika Mungu ni Mkubwa

 

Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya
Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi Emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100, Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia Jumamosi muda wa saa sita na nusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya Mafiati Mbeya wengi wa mashuhuda hao, walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo.
Hii ndiyo hali halisi, iliyotokea siku hiyo ya ajali, timu ya blogu ya Mbeya Yetu mabayo matukio haya, bayana blog imeyapata kutoka kwake, ilipofika usiku huo, eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ndipo jana ikaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda, ili akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo timu hiyo, ikaenda kufuatilia harusi hiyo katika kanisa la Agape.
Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani
Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa.
Sasa bwana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa.
Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T DSM, ndiyo aliyefungisha ndoa hiyo
Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru Mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea.
Hapa wakipata baraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa la AGAPE
Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe.
Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota
Wakitoaka kanisani baada ya ndoa yao kufungwa
Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa, wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea kwenye ukumbi wa reception.
Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao
Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya CCM, jijini mbeya
Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo, ingawa maharusi hawakuweza kufika kwenye sherehe hiyo, kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu.



Ndugu, jamaa na marafiki wakipata chakula. (Picha zote na Gwasa wa Mbeya yetu)


 

No comments:

Post a Comment