Rais Jakaya Kikwete (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Steve Kilindo cheti cha kutambua mchango wa kampuni hiyo kufanikisha hafla ya
kuvizawadia viwanda Tuzo ya Rais ya Uzalishaji Bora viwandani 2012, katika
hafla iliyofanyika juzi kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Viongozi wa TBL
wakishangilia baada ya kukabidhiwa cheti hicho. Kampuni hiyo ilifadhili vinywaji
kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania
(CTI).
Viongozi hao wa TBL waliohudhuria hafla hiyo, wakinywa vinywaji baada ya kugongeana glasi kutakiana heri. |
Viongozi hao wakiwa
wamesiamam wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya TBL,
Arnold Kilewo (kushoto) na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa kampuni hiyo,
Steve Kilindo wakipata mlo wa usiku.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris
Malulu (kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kupata
maakuli.
Rais Jakaya Kikwete
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries
Limited (TDL), kikombe cha ushindi wa jumla wa tuzo hizo za Rais. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Bodi ya TBL, Kilewo. TDL ni kampuni tanzu ya TBL. (Picha zote na Kamanda wa Matukio Blog)
No comments:
Post a Comment