TANGAZO


Thursday, December 27, 2012

Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa alivyowapagawisha Kivule Sikukuu X-Mas

 

Malkia wa Mipasho Khadija Kopa, akionesha ufundi wake wa kunengua wakati alipokuwa akiimba maarufu wa 'Mimi ndiye Queen' katika onesho la kundi la TOT Plus lililofanyika Kivule, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni onesho la X-Mas. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

Umati wa mashabiki ukijimwaya ukumbini kwenye kitongoji cha Kivule, jijini Dar es Salaam, kuzirudi ngoma za kundi hilo.

Shabiki akishindwa kujizuiya na kujikuta akivamia jukwa kwenda kumtunza fedha, malkia huyo wa mipasho, bibie Khadija Kopa.

Mashabiki, wa kike na kiume wakisigana kwenye ukumbi huo katika kitongoji cha Kivule, jijini Dar es Salaam kuzirudi ngoma za kundi hilo.

Khadija Kopa, 'Malkia wa Mipasho' (katikati), akizirudi ngoma pamoja na mashabiki wake katika onesho hilo.

Khadija Kopa akiwa kazini akiimba nyimbo inayoitwa 'Huniwezi', wakati wa onesho hilo.

No comments:

Post a Comment