TANGAZO


Thursday, December 27, 2012

Mzee Yussuf na kundi lake la Jahazi walivyopasua usiku wa Boxing Day, Dar Live, Mbagala

 



MzeeYusuf na kundi lake la Jahazi Modren Tarab, akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, usiku wa 'Boxing Day'.
 


Mke wa Mzee Yusuf, Leila Rashid, akizikonga nyoyo za wapenzi wa taarab usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
 


Dada wa Mzee Yussuf, Khadja Yusuf, akiwachizisha wapenzi wa taarab ndani ya Dar Live.
 


Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Fatma Mahmoud 'Mcharuko', akiwapa raha mashabiki.
 


Umati wa mashabiki, uliohudhuria shoo hiyo kali kutoka Jahazi Modern Taarab, ukizirudi ngoma hizo za Jahazi.
 


Mzee Yusuf 'on stage', akiongea na mashabiki wake, ukumbini humo.
 


Khadja Yusuf naye kazini, akirudia kutumbuiza kwenye jukwa la ukumbi huo.
 


Bi. Leila Rashid, makamuzi yakiendelea ukumbini humo.
 


Mzee Yusuf hakuchoka kuwapa mashabiki wake burudani ndani ya Dar Live.
 


Wapenzi wa taarab wakijiachia kwa raha zao, kuzirudi ngoma hizo za kundi la Jahazi.
 


Sehemu ya umati wa mashabiki, uliojazana ukumbini humo wakati wa onesho hilo, la usiku wa Boxing Day, wakizirudi ngoma za kundi hilo.
---
KUNDI la Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake, Mzee Yusuf ' Mfalme' usiku wa 'Boxing Day', lilifanya makamuzi ya nguvu ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzikonga nyoyo za wapenzi wa taarab waliofurika mahali hapo. (Picha zote na Issa Mnally na Richard Bukos/GPL)


No comments:

Post a Comment