TANGAZO


Saturday, December 15, 2012

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, yakutana mjini Zanzibar



Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa ya Zanzibar, wakipitia ajenda za kikao katika ukumbi wa CCM, Kisiwandui Mjini Zanzibar leo, katika kikao cha siku moja, chini ya Mwenyekiti wake, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk.Ali Mohamed Shein, ikiwa ni kikao chake cha mwanzo tokea kushika nafasi hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama Uliofanyika Mjini Dodoma.

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abrahman Kinana (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wakiimba wimbo wa Chama wakati Rais Shein, alipowasili katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui, katika Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika leo.

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abrahman Kinana, wakati Rais Shein alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui, kushiriki katika kikao cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, mjini humo leo.

Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, wakiwa katika Kikao maalum katika ukumbi wa CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo, katika kikao cha siku moja. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar)


No comments:

Post a Comment