TANGAZO


Saturday, December 15, 2012

Vijana Jazz waibuka upya, wapakua mbili moto wa kuotea mbali, Wamimina shukurani kwa Rais Kikwete kuwapatia vyombo vipya, Zilipendwa zawakonga mashabiki Masae Bar, Kawe

 
Picha tofauti za wanamuziki wa Vijana Jazz wakiwajibika jukwaani katika ujio mpya wa bendi hiyo, ukumbi wa Masae, Kawe jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Wanamuziki wa kundi hilo, wakizirudi ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza ukumbi wa Masae Bar, Kawe jijini Dar es Salaam.
 
Mmoja wa waimbaji wa kundi hilo, akiwajibika kwenye onesho hilo.
 
Mwimbaji Abdallah Mgonahazelu akiimba wakati wa onesho hilo.
 
Mwimbaji Nuru Mhina 'Baby White', akiimba wakati wa onesho hilo.
 
Mwimbaji Roshi, akiwa kazini katika onesho hilo, ukumbi wa Masae Bar, Kawe jijini.
 
Mpuliza Sexaphone (mdomo wa bata), akiwajibika jukwaani katika onesho hilo.
 DAR ES SALAAM, Tanzania
BAADA ya kuwa 'juu ya mawe' kwa muda mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya Vijana Jazz, 'Wana Air Pambamoto', imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa ikiipua vibao viwili vipya, kusuuza nyoyo za mashaki wake.
Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Masae Bar, Kawe Wilaya ya Kinodoni, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, bendi hiyo, imedhihirisha kwamba bado ni moto wa kuotea mbali na kwamba mashabiki wake wengi bado wapo.
 
Ikitumbuiza kwenye ukumbi huo, unaotazamana na kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packes, Vijana Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa kupiga nyimbo zake za zamani zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi', 'Ngapulila' na 'mawifi', zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo, marehemu Ahmed Maneti katika miaka ya 1980.
Nyimbo hizo, ziliwapeleka puta mashabiki wa bendi hiyo na kuwafanya kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba sambamba na wanamuziki waliovuokuwa wakiimba jukwaani na wengine kwenda jukwaani kutuza waimbaji.
Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri, wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.
Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua ni 'Utanieleza nini', utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani alisema, nyumbo hizo zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.
Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo hizo kwa ajili ya kiusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi imo katika jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.
 
"Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa Kikweye. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema Mgonahazeru wakati kabla ya bendi hiyo kuanza kuiba wimbo wao mpya wa 'Utanieleza nini'.
Vijana Jazz ni moja ya bendi ambazo Mratibu wa Budurano zote kwenye ukumbi huo wa Masae, Juma Mbizo, amesema atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'.

No comments:

Post a Comment