TANGAZO


Saturday, December 8, 2012

Francis Miyeyusho, Nasibu Ramadhan wapima uzito


Bondia Said Mundi wa Tanga (kushoto), akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe', baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho, Jumapili Desemba 9, ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es Salaam.

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe', akipimwa afya na Dk. Kalaga wakati wa maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake na Saidi Mundi wa Tanga (wa pili kulia), wengine kulia ni Promota wa mpambano huo, Mohamed Bawazir na wa pili kushoto ni Mratibu wa mpambano huo, Paul Kunambi.

Promota ya mpambano wa masumbwi, Mohamed Bawazir (katikati), akiwa na baadhi ya mabondia wakati wa kupima uzito.
 

B
aadhi ya mashabiki, wakishangilia wakati wa upimaji uzito wa mabondia watakaopambana katika ukumbi wa PTA, Saba Saba siku ya Jumapili Desemba 9, jijini Dar es Salaam.

Bondia Francis Miyayusho akipima uzito kwa ajili ya kumkabili Nassibu Ramadhani (kushoto), katika mpambano wao wa kuwania ubingwa wa WBF, utakaofanyika kesho Jumapili, Disemba 9, ukumbi wa PTA Sabasaba jijini.

Bondia Nassibu Ramadhani (kushoto), akitunishiana msuli na bondia Fransic Miyeyusho wakati wa uipimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho, Desemba 9.
 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe', akipima uzito kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake, Said Mundi (kushoto), mpambano utakaofanyika kesho, Desemba 9, jijini Dar es Salaam.
 
Bondia Said Mundi wa Tanga (kushoto), akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao, utakaofanyika kesho Jumapili Desemba 9, ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es Salaam. (Picha zote kwa hisani ya: www.superdboxingcoach.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment