Waziri wa Habari ,Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, akizungumza na Ujumbe wa wandishi wa habari kutoka nchini Misri huko Wizarani, mjini Unguja leo. Wandishi hao, walitembelea maeneo kadhaa ya Kiutalii Zanzibar.
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 07/11/2012
Waziri wa
Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk amesema kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzíbar inakusudia kuifanya sekta ya utalii kuongeza nafasi za
ajira kwa wananchi wake ili kuinua kipato chao na Taifa kwa
ujumla.Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 07/11/2012
Hayo ameyasema leo, huko Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo wakati alipokutana na Waandishi wa Habari kuto nchini Misri waliofika Zanzíbar kujionea shughuli mbalimbali za utalii zinavyofanywa na kuweza kuitangaza Zanzíbar katika nchi ya Misri.
Amesema hali hiyo
itafikiwa kwa kuwepo misingi imara ya uwekezaji na kupokea watalii
wa daraja la juu ambao wana nafasi kubwa ya kuongeza ajira katika maeneo ya
mijini na vijijini ili kuondoa umasikini .
“Unapolikuza soko
la utalii nikutangaza utalii hivyo ni matumaini yetu kuona tuna pokea watalii
wenye kipato ambao watatoa ajira zaidi katika nchi” alisema Waziri
Mbarouk.
Aidha, Waziri huyo
alisema kuwa suala hilo litafanikiwa kutokana na kuimarishwa miundo mbinu ya
uwekezaji,fukwe zilizo bora, hoteli za kimataifa na mashirikiano mazuri
yanayofanywa na wadau wa sekta hiyo ikiwemo mashirika ya ndege ,watembezaji
wageni na wawekezaji wa mahoteli.
Alisema hiyo ni
nafasi ya kipekee kwani itaongeza nafasi za ajira kwa Wananchi na kupelekea
kukua kwa uchumi wa taifa mbapo sekta ya utalii ndio muhimili mkuu wa uchumi
kwasasa.
Nae Mkurugenzi
Jumuiya ya uwekezaji utalii Zanzíbar (ZATI) Julia Bishop alisema kuwa
wanaishukuru sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar kwa kuwapa mashirikiano
kikamilifu jambo linalopelekea sekta ya utalii kuimarika bila ya pingamizi.
Julia alisema kwa
upande wao wanafanya kazi kubwa kuitangaza Zanzíbar kupitia sekta ya utalii
ambapo pia hufaidika pale wageni wanapoingia nchini .
Nae mkuu wa msafara
kutoka Ubalozi wa Misri Mwandishi Marwa Taufik alimuelezea Waziri Mbaruok
kuridhishwa kwao na mapokezi sambamba na kujua jinsi gani Serikali ya Mapinduzi
ilivyojipanga vyema katika kuendeleza sekta ya Utalii nchini.
Tawfik alimuahidi
Waziri huyo kuitangaza Zanzíbar kiutalii katika nchi yao ya Misri kutokana na
mazingira mazuri ya kiutalii ambayo Zanzíbar imejaaliwa kulinganisha na nchi
nyingine.
No comments:
Post a Comment