Rais Barack Obama |
Rais Jakaya Kikwete |
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza furaha na
shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumanne, Novemba 6, 2012 wa Rais Barack
Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.
Katika salamu zake za
pongezi kwa kiongozi huyo wa Marekani ambaye amechaguliwa tena na wananchi wa nchi
hiyo kwa kipindi cha pili, Rais Kikwete amesema mapema leo, Jumatano, Novemba
7, 2012:
“Nimepokea kwa furaha
na shangwe habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa Marekani kwa kipindi
cha pili. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
na kwa hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe na kupitia
kwako Chama cha Democratic pongezi nyingi kwa ushindi wako wa maana sana.”
Ameongeza Rais
kikwete katika salamu zake hizo: “Kuchaguliwa kwako tena kuendelea kuongoza
nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi ya uaminifu na imani
ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi wako wa mfano.”Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua tena uongozi wa nchi hiyo katika kipindi chako kipya, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi na ule wa Serikali yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa na wewe na Serikali yako ya kutukuka, ili kuendeleza uhusiano bora ulioko kati ya nchi zetu mbili ndugu.”
No comments:
Post a Comment