Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Alhaji Omar Mussa Sheha (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa kijiji cha
MahembeKata ya Sawida Wilayani Etilima mkoani Simiyu kabla ya kuanza kwa mkutano
wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume hiyo leo
jumanne tarehe 27. Novemba, 2012. Wengine kutoka kulia ni wajumbe wa Tume hiyo,
Yahya Msulwa, Jesca Mkuchu na Said El-Maamry.
Mjumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Alhaji Said El- Maamry (aliyesimama) akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Mahembe Kata ya Sawida Wilayani Itilima mkoani Simiyu
kabla ya kuanza kwa mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya
ulioitishwa na Tume hiyo leo jumanne, Nov. 27, 2012. Wengine pichani ni wajumbe
wa Tume, kushoto Yahya Msulwa, kulia Alhaji Said El-Maamry na Jesca
Mkuchu.
Mkazi wa
Kijiji cha Inaro Kata ya Luguru Wilayani Itilima mkoani Simiyu, Pius Ndaki (36)
akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo leo Jumanne Nov. 27, 2012.
Mkazi wa
kijiji cha Inaro Kata ya Luguru Wilayani Itilima mkoani Simiyu, Bw. Malanda
Madeleja (30) ambaye ni mlemavu wa miguu akitoa maoni yake kuhusu Katiba wakati
wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo leo Jumanne
Nov. 27, 2012.
Mjumbe wa
Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Yodos Mandera akiwapatia fomu
maalum za kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mahembe
iliyopo kijiji cha Mahembe Wilayani Itilima mkoani Simiyu mara baada ya kufika
na kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo, Jumanne Nov. 27,
2012.
Mjumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jesca Mkuchu (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa
vifungu vya Katiba kwa wananchi wa kijiji cha Inaro Kata ya Luguru Wilaya ya
Itilima mkoani Simiyu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kutoa maoni kuhusu Katiba
Mpya ulioitishwa na Tume hiyo leo, jumanne Nov. 27, 2012. Wengine pichani ni
wajumbe wa Tume, kushoto Omar Mussa Sheha, Yahya Msulwa na Alhaji Said
El-Maamry.
Mkazi
wa kijiji cha Inaro, Kata ya Luguru wilayani Itilima, mkoani Simiyu, Bw. Enock
Mussa (24), akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Kijijini hapo leo Jumanne Nov. 27,
2012.
Akinamama
wa kijiji cha Mahembe Kata ya Sawida Wilayani Itilima mkoani Simiyu wakijisomea
nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi
kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume hiyo, leo Jumanne Nov. 27,
2012.
Na Ismail
Ngayonga, Simiyu
MKAZI wa kijiji cha Inaro,
Kata ya Luguru Wilayani Itilima mkoani Geita, Amos Kuhoka (30)amependekeza
Katiba Mpya iweke sheria ya kutoa ruzuku kwa Wajawazito wanaokwenda kujifungua
watoto katika vituo vya afya nchini.
Akitoa maoni yake leo
(jumanne Nov. 27, 2012) kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema
moja ya vifungu vya katiba ya sasa vinatamka wazi kuhusu haki ya kuishi kwa
binadamu, hivyo wazazi ni lazima wasaidiwe katika malezi ya watoto
hao.
Akifafanua zaidi alisema
katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka matukio mbalimbali ya wanawake kutoa
mimba, hivyo kusababisha kukatisha uhai wa mtoto aliyetarajiwa kuzaliwa. “Katiba
Mpya itamke wazi kuwa Mama anapewa ruzuku kama zawadi anapokwenda kujifungua ili
aweze kumlea vyema mtoto wake” alisema.
Naye Bw. Amos Kuhoka (30)
ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, alipendekeza Katiba Ijayo iwasaidie watoto
wanaozaliwa majumbani nao pia kuweza kupata vyeti vya kuzaliwa tofauti na ilivyo
sasa kwani vyeti hivyo hutolewa kwa watoto wanaozaliwa katika mahospitali
pekee.
“Kwa kweli huwezi kufahamu
uchungu wa Mama katika kujifungua utampata wapi, kokote unaweza kumfika hata
nyumbani pia hivyo ni vyema katika Katiba kuwepo na kipengele kinachowasaidia
watoto wanaozaliwa nyumbani nao kupata vyeti vyao vya kuzaliwa”
alisema.
Aidha, alisema kuwa wazazi
wengi wenye watoto waliojifungulia nyumbani ambao wana uwezo mdogo wa kifedha
wamejikuta wakishindwa kuvipata vyeti hivyo na kuwafanya watoto wao kuishi
pasipo kuwa na vyeti hivyo.
Kwa upande wake Bw. Lameck
Lazaro (43), amvaye naye pia ni mkazi wa kijiji hicho naye amependekeza Katiba
Mpya iweke kipengele kitakachowawezesha wazee wenye umri wa miaka 60 na
kuendelea kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.
Alisema katika miaka ya hivi
karibuni kumekuwepo na usumbufu wa mara kwa mara unaojitokeza kuhusu umri halisi
wa wazee nchini.
Aliongeza kuwa wazee wengi
wameshindwa kutambua uhalisia wa umri walionao kwa kuwa walizaliwa katika miaka
ya zamani ambapo hakukuwa na utaratibu wa kuandisha cheti cha kuzaliwa na badala
yake wengi wao wamekuwa wakibahatisha kuhusu umri alianao.
“Katiba Mpya itamke wazi kuwa
wazee wote watapatiwa vyeti vya kuzaliwa ili kuwasaidia kutambua umri wao”
alisema.
No comments:
Post a Comment