Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka
(kulia), akiongozana na mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro ambapo katika harambee hiyo jumla ya
shilingi milioni 278 zilipatikana.
Mwenyekiti wa Bodi ya
wakurugenzi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi akizungumza
katika harambee hiyo.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu
wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akipokea mchango wa shilingi milioni
tatu kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
ukiwa ni mchangop wake kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa
kike wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi waliochangia harambe hiyo, akimpa mkono mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro.
Meneja
Mawasiliano wa TCRA, Inocent Mungi akikabidhi mchango wa shilingi milioni tano
kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro wakati wa
harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa
kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau
waliojitokeza katika harambee hiyo
Mwanasheria wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, Vupe Ligate akipeana mkono na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa
Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro baada ya kuchangia katika harambee ya
ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike ambapo jumla ya shilingi milioni 278
zilipatikana katika harambee hiyo.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu
wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Rex
Energy, Francis Kibisa kwa mchango alioutoa katika harambee ya kuchangia ujenzi
wa mabweni ya wanafunzi wa kike.
Naibu
Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro (katikati) mfano wa
hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha
Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Christiane Manyeye (kulia) na mwakilishi wa
ubalozi wa Kenya, Boniface Makao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es
Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.
Shukuru Kawambwa.
Miss
Tanzania 2005, Nancy Sumari akikabidhi mchango wa dola za kimarekani 1,000 kwa
Aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose
Migiromgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa
mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mstaafu Dk.
Asha Rose Migiro (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkuu
wa Kitengo cha mahusiano wa Shirika
la Nyumba (NHC), Susan
Omari baada
ya shiriki hilo kuchangia mabati 1,000 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa
ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wasanii wa kundi la
THT wakitumbuiza katika harambee hiyo.
Mkurugenzi wa
Radio One, Deogratius Rweyunga akipokea cheti cha shukrani kutoka
kwa Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa
mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmiliki
wa Blog ya 820, Shamim Mwasha, akitoa mchango wa shilingi laki 6.5 alizokusanya
kutoka kwa wasomaji wa mtandao wake.
No comments:
Post a Comment